BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)

TAARIFA KWA UMMA 

MATOKEO YA UHAKIKI WA UDAHILI AWAMU YA KWANZA KATIKA 
PROGRAMU MBALIMBALI KWA MKUPUO WA SEPTEMBA 2023/2024


BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)




Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) 
linautaarifu umma kuwa matokeo ya uhakiki wa sifa za walioomba kujiunga na
programu mbalimbali kwa awamu ya kwanza kwa mkupuo wa Septemba 2023/2024
yametoka rasmi leo tarehe 28 Julai, 2023.
Udahili kwa mwaka wa masomo 2023/2024 ulianza tarehe 21 Mei, 2023 hadi tarehe 16 Julai, 
2023. Waombaji wa programu za Astashahada na Stashahada walituma maombi ya kudahiliwa 
katika vyuo mbalimbali Tanzania Bara na visiwani. Vyuo vilipokea maombi ya waombaji kisha 
kufanya uchaguzi kulinganana sifa za programu zinazotolewana vyuo hivyo. 
Jumla ya wombaji 24,774 kutokavyuo 165 walichaguliwa na vyuo, na kuwasilishwa NACTVET
kwa ajili ya uhakiki kuanzia tarehe 17 - 21 Julai, 2023. Waombaji 22,729 sawa na (92%) ya 
waombaji wote (wanawake ni 11,910 (52%) na wanaume 10,819 (48%) wamekidhi vigezo vya 
kujiunga na programu walizochagua. 
Aidha, jumla ya waombaji 1,922 sawa na (8%) ya waombaji wote hawakuwa na vigezo vya 
kujiunga kwenye programu walizochagua, wanawake ni 972 (51%) na wanaume ni 950 (49%). 
Majina ya waombaji waliohakikiwa tayari yametumwa vyuoni.
Waombaji wote waliowasilishwa NACTVET kwa ajili ya uhakiki wametumiwa 
ujumbe na msimbo (code) kupitia namba za simuzilizowasilishwa na vyuo.
Msimbo huo utatumika kuhakiki udahili wao na sifa kwenye programu
walizochaguliwa kupitia tovuti ya NACTVET www.nacte.go.tz kwa kubofya 
kitufe cha “Verification results 2023”.
Waombaji waliohakikiwa na kuonekana kuwa hawakukidhi vigezo kwenye
programu walizoomba, wanashauriwa kuomba programu zingine wakati wa 
awamu ya pili itakayoanza tarehe 28 Julai hadi 10 Septemba, 2023.
Matokeo ya uhakiki kwa awamu ya pili yatatolewa tarehe 2 Oktoba, 2023. 
Masomo kwa waliochaguliwa yataanza rasmi tarehe 16 Oktoba, 2023. 

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)
28/07/2023

Post a Comment

0 Comments